Wanachama wa Ufipa cooperative union wa Matanga women Amcos na Mbala AMCOS iliyopo laela wakumbwa na janga la mvua ya mawe iliyoharibu Mazao Yao zaidi ya ekari 50. Mvua hiyo ilinyesha jumapili ya tarehe 12/02/2023. Hata hivyo bank ya Nmb ambao ndio waliowakopesha mkopo wa kilimo wameanza ziara ya kuwatembelea wahanga ili kufanya tathimini ya janga hilo. Hii nikutokana na mashamba ya wanaushirika kukatiw bima ya kilimo. Akilizungumza na wakulima wake mwenyekiti wa Ufipa cooperative union Bw Adabeth Mbuyani ameelezea kuwa wakulima wanaolima kilimo biashara wanapaswa kujifunza umuhimu wa kuwa na bima ya majanga ili kunusuru mitaji Yao pindi majanga yanapojitokeza.
Hata hivyo Bado Ufipa cooperative union wanatarajia kuwa na mavuno Mengi zaidi ya Mazao Yao kwa mwaka huu 2023 ukilinganisha na msimu uliopita.