Bodi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani imefanya kikao tarehe 16.03.2023 na Bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa wa Rukwa (Ufipa Cooperative Union – UCU) Kwa lengo la kujadili namna ya uendeshaji wa mfumo katika mkoa wa Rukwa.
Uanzishaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ndani ya Mkoa wa Rukwa umekwisha tiwa baraka na uongozi wa Mkoa kwani utaleta mapinduzi ya masoko ya mazao ya wakulima kwani tatizo la soko limekuwa la Muda mrefu sana. Wakulima wa Mkoa wa Rukwa wapo tayari na wameonyesha nia ya dhati kuupokea mfumo huu. kwa upande wa chama kikuu cha ushirika UCU kama watekelezaji wakuu wa mfumo, wameweka makubaliano na Bodi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuwajibika ipasavyo ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwainua wakulima wa Mkoa wa Rukwa.