Akielezea namna wanaushirika waliopo Mkoa wa Rukwa Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo Bw Hance Sampala ameelezea kuwa musimu huu wa kilimo wanaushirika wamenufaika vyema na Mbolea za ruzuku. Lakini pia ameelezea namna wanavyojipanga kwa msimu ujao kuwa wapo kwenye mikakati ya kuhakikisha wanaviingiza vyama vya ushirika kuwa mawakala wa pembejeo kwa msimu ujao wa kilimo ili kusogeza huduma kwa wakulima waliopo vijijini.